Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Moses Sabalua,
Vijana katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii ipasavyo.
Kwa mujibu wa mchungaji wa kanisa la Kenya Assembly of God (KAG) mjini Marsabit Joseph Mwendwa, ni kuwa vijana wanauwezo wa kutumia mitandao kwa njia ambayo inawafaidi na wala sio kueneza chuki au maovu.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee mchungaji Mwendwa amewahimiza vijana kutumia mitandao kukuza talanta zao pamoja na njia zingine ambazo zinaweza kuwapa mapato.
Aidha mchungaji Mwenda amewataka vijana kuwa waangalifu wanapotumia mitandao kwani kuna walaghai pia wanawahadaa watu kupitia mitanda au hata kuwaelekeza katika njia potovu.