Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng,
Vijana wa kanisa Katoliki hapa jimboni Marsabit wameshauriwa kuwa na mazoea ya kushiriki katika ibada pamoja na halfa ambazo zinaangazia neno la Mungu.
Ni ushauri ambao umetolewa na mwenyekiti wa vijana wa katoliki eneo la Sagante, Parokia ya Cathedrali, jimboni Marsabit, Gabriel Galgallo Boru ambaye amesema kuwa vijana waKatoliki wanauvivu wa kusoma Biblia jambo ambalo ameLItaja kuwa linalemaza na kuyumbisha Imani ya vijana wengi jimboni.
Boru ameelezea kuwa ni jukumu la kila kijana kuhakikisha kwamba amepata muda wa kushiriki katika warsa za kuchambua Biblia ili kuweza kuelewa zaidi kuhusu mafunzo matakatifu na kuimarisha Imani yao.
Aidha Boru ametaja umitumizi ya mitandao na vilevile uraibu wa dawa za kulevya na mihadarati kama changamoto kuu ambazo zinawafanya vijana kutotilia maanani mafundisho ya Biblia.
Wakati uo huo Maria Orge ambaye pia ni kiongozi wa vijana wa Katoliki eneo la Sagante, amewataka vijana kutumia fursa hii ambayo kanisa linasherehekea Jubilee ya mwaka wa matumaini kuweza kuwatia wenzao moyo wa kusoma na kuielewa Biblia.