County Updates, Local Bulletins

VIJANA 42 WALIOTUMA MAOMBI YA KUPATA VITAMBULISHO VYA KITAIFA JUMAMOSI WIKI JANA WATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO KATIKA KITUO CHA HUDUMA CENTER MJINI MARSABIT.

Naibu Kamishna wa Marsabit Central David Saruni, Machifu wa Marsabit Central pamoja na maafsa kutoka afisi ya usajili Marsabi wakipeana kitambulisho

Na JB Nateleng,

Vijana 42 waliotuma maombi ya kupata vitambulisho vya kitaifa Jumamosi wiki jana wakati wa ziara ya mkuu wa utumishi wa umma nchini Felix Koskei pamoja na katibu katika idara ya uhamiaji Bellio Kipsang katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuchukua vitambulisho vyao katika kituo cha Huduma center hapa mjini Marsabit.

Akizungumza na idhaa hii mkurugenzi wa kituo cha Huduma Center tawi la Marsabit Geofrey Ochieng amesema kuwa ni jukumu la wazazi kuhakikisha kuwa wanao ambao wametimiza umri wa miaka 18 wanapata vitambulisho vya kitaifa huku wakilenga kuzuru shule zote jimboni ili kuwapa wanafunzi walio na umri wa miaka 18 vitambulisho.

Viongozi hawa (Felix Koskei na Bellio Kipsang) walizuru kaunti ya Marsabit Jumamosi kwa madhumuni ya kuzindua rasmi mtambo ambao utarahisisha mchakato wa kupata vitambulisho kutumia mfumo wa kidijitali, hatua ambayo viongozi wa serekali jimboni wameweza kuishabikia na kuitaja kama ya manufaa zaidi kwa wanaMarsabit.

Subscribe to eNewsletter