Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Caroline Waforo,
Huku Kenya ikijiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya uhuru wa wanahabari hapo kesho tarehe 3 mwezi Mei washikadau mbalimbali nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanalinda uhuru wa vyombo vya habari.
Ni wito ambo umetolewa na mratibu wa Baraza la vyombo vya habari nchini MCK katika eneo la kati na mashariki mwa nchi Jackson Karanja ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu.
Karanja anasema kuwa kulinda uhuru wa wanahabari kunafaa kupewa kipaumbele ikikumbukwa kuwa uhuru wa wanahabari nchini unazidi kupuuzwa kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Aidha Karanja anasema kuwa baraza la vyombo vya habari nchini linafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa uhuru wanahabari na vyombo vya habari unalindwa kwa kuandaa mikutano baina ya wanahabari na wadau mbalimbali kama njia ya upatanishi na kutengeneza uhusiano mwema.
Vile vile mratibu huyu amevitaka vyanzo vya habari kuwa na wepesi wa kutoa taarifa haswa serikali za majimbo.
Karanja hata hivyo amesisitiza umuhimu wa ushirikaino kati ya serikali, vyombo vya habari pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo na kijamii ili kuhakikisha kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Uhabarishaji kwenye Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba maanuru AI kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari” ikilenga kuonyesha namna dunia inavyobadilika kwa kasi kwa sababu ya maendeleo ya teknolojia hasa teknolojia ya akili mnemba ukipenda AI.