County Updates, Local Bulletins

TUME YA KUWAAJIRI WALIMU NCHINI YATOA ORODHA YA WALIMU WALIOPANDISHWA NGAZI.

Na Joseph Muchai,

Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC imetoa orodha ya walimu waliopata kupandishwa daraja kote nchini.

Hili linafuatia mahojiano yaliofanyika kati ya tarehe 7 mwezi januari na tarehe 6 mwezi februari mwaka huu kwa shule za secondari na vyuo vya anuai.

Aidha mahojiano mengine yalifanyika kati ya tarehe 13 mwezi Januari na tarehe 23 januari mwaka huu kwa walimu wa shule za msingi.

Kulingana na taarifa kutoka tume hiyo tawi la Marsabit idadi kubwa ya walimu wamepandishwa daraja ila bado wanangojea kupata barua kutoka kwa tume hiyo.

Hatua hii ya TSC inajiri mwaka mmoja tangu kuwapandisha vyeo walimu wengine mwaka jana.

Hata hivyo tume hiyo inasema kwamba ina upungufu wa walimu wa shule za sekondari ya msingi JSS.

TSC huandaa zoezi la kuwapandisha walimu vyeo kila mwaka kama njia moja ya kuwapa motisha na kuwazawadi walimu kwa juhudi zao za kutoa huduma katika idara ya elimu.

Subscribe to eNewsletter