Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Hendry Khoyan
Tahadhari imetolewa kwa wazazi na walimu wa lokesheni ya Songa, kuwa wangalifu haswa msimu huu wa mvua na kuwazuia wanao kucheza karibu na shimo kubwa lililopo kati ya eneo la Songa na Lpus, linalojulikana kama ‘Mugur Eletipo’.
Kwa mujibu wa naibu wa Chifu wa lokesheni ya Songa, Luka Lolkipayangi aliyezungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu, ni kwamba watoto, hasa wanafunzi, wanapenda kutembelea eneo hilo kucheza jambo linaloweza kuhatarisha maisha yao.
Chifu Lolkipayangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwazuia watoto wao kutembelea eneo hilo ili kuepusha ajali na hatari inayoweza kutokea huku akiirai jamii kushirikiana ili kulinda watoto na kuhakikisha usalama wao katika kipindi hichi cha mvua.
Naibu chifu huyo amewasihi walimu pia kushirikiana ili kuzuia hatari inayoweza kutokea na vilevile kuwataka kutatua changamoto hiyo.
Kulingana na naibu wa chifu huyo, shimo hilo lina kumbukumbu za kusikitisha kwani katika miaka ya nyuma, mtoto mmoja wa miaka saba alipoteza maisha yake katika mazingira ya kutatanisha baada ya kucheza karibu na shimo hilo.