Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya
Mashahidi kutojitokeza kutoa ushahidi kortini katika kaunti ya Marsabit kunalemaza kesi za dhulma za kijinsia.
Haya yamewekwa wazi na afisa wa watoto katika kauti ya Marsabit Mukanzi Leakey.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani, Mukanzi amesema kwamba wahalifu haswa wa dhulma ya kijinsia wanasalia huru hata licha ya wao kufanya makosa kutokana na idadi kubwa ya mashahidi kukosa kufika mahakamani kutoa ushahidi jambo linalolemaza kesi dhidi yao na kupelekea mahakama kuwaachilia huru.
Aidha Mukanzi amewahakikishia mashahidi usalama wao haswa iwapo watatoa ripoti muhimu kwa idara ya DPP ambayo imeweka mikakati dhabiti ya kuwalinda mashahidi dhidi ya hatari zozote.
Vilevile Mukanzi ameonya dhidi ya kutatua kesi za unajisi kupitia wazee huku akisema kuwa watakao husika katika kutatua kesi zozote za dhulma za kijinsia kupitia wazee watachukuliwa hatua kali za kisheria kwani kesi hizo zinafaa kutatuliwa mahakamani.