Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Caroline Waforo
Huku wafanyikazi wa serikali ya kaunti wakilalama kuchelewa kwa mishahara ya miezi miwili sasa serikali ya kaunti ya Marsabit inasema kuwa kuchelewa kwa mishahara hiyo ni kutokana na serikali kuchelewesha mgao wa fedha kwa serikali za kaunti kote nchini.
Akizungumza na radio jangwani wakati wa kipindi cha Amkia Jangwani Jumatano Msemaji wa serikali ya kaunti ya kaunti ya Marsabit Abdub Barille anasema kuwa wafanyikazi wanadai serikai ya kaunti mishahara ya mwezi wa Februari na Machi akisema kuwa ni changamoto inayoshuhudiwa sio tu Marsabit bali nyingi ya kaunti nchini.
Siku ya Jumanne madaktari kupitia muungano wao wa KMPDU tawi la Marsabit walisema kuwa kuchelewa kwa mishahara ni mojawapo ya sababu ambazo zimewapelekea wao kushiriki mgomo ambao umeingia siku yake ya tisa leo hii.
Maswala mengine ni ukosefu wa bima ya afya pamoja na kutowasilishwa kwa makato kwa taasisi mbalimbali.