Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Caroline Waforo
Serikali ya kaunti ya Marsabit imelaumiwa kwa kuzembea katika kutatua maswala yanayowaadhiri madaktari jimboni.
Kulingana na afisa wa shughuli za KMPDU kaunti ya Marsabit Dr Isaac Karogu ni kuwa serikali ya kaunti imekuwa ikipuuza maslahi ya madaktari kwa kukosa kutekeleza makubaliano ya kurejea kazini pamoja na mikakati ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi yaliyoafikiwa kati ya KMPDU na serikali ya kaunti ya Marsabit mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu Dr Karogu amesema kuwa hili limepelekea madaktari hao kushiriki mgomo ambao umeingia siku yake ya nane leo Jumanne huku madaktari wakisema wakisema kuwa mgomo huo utaendelea hadi wakati ambapo maslahi yao yatakapoangaziwa.
Kulingana na Dr Karogu mgomo huo ulianza baada ya kutamatika kwa makataa ya wiki mbili.
Madaktari wanaidai serikali ya kaunti ya Marsabit mishahara ya miezi miwili huku pia wakilalama makato kutowasilishwa kwa taasisi mbalimbali. Mwishoni mwa mwaka jana kamati maalum iliundwa kuchunguza matakwa ya wafanyikazi wa kaunti jambo analosema Dr Karogu kuwa ripoti ilitolewa ila haijawasilishwa kwa baraza la mawaziri wa kaunti ya Marsabit ili kujadiliwa.
Madaktari hawa wamelalamikia ukosefu wa bima ya matibabu ambapo kulingana na Dr Karogu wanaendelea kupitia ugumu katika juhudi za kutafuta matibabu.
Pia wamelalamikia kutowasilishwa kwa makato wanayokatwa na bima ya matibabu ya taifa care chini ya bima ya SHA na hivyo kuwafanya kukosa huduma za matibabu.
Muungnao huu wa Madaktri unasema kuwa katibu katika serikali ya kaunti ya Marsabit aliwaambia madaktari jimboni kuwa serikali ya kaunti itasuluhisha maslahi yao japo wanasema kuwa hawakuridhika baada yake kukosa kutoa muda kamili ambapo maswala yao yataangaziwa.