KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na JB Nateleng
Serekali kuu kupitia idara ya maeneo kame na ustawi wa miji inaendelea kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo katika eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit
Kwa mujibu wa katibu katika idara ya maeneo kame na ustawi wa miji Kello Harsama ni kwamba serekali imeweza kuhakikisha kuwa wakazi wa eneo bunge la Laisamis wameweza kunufaika na mradi wa maendeleo ambao unajumuisha kupewa chakula pamoja na kuchimba visima vya maji kwa ajili ya mifugo na mahitaji wa wakazi kwa ujumla.
Akizungumza alipozuru eneo la LogLogo eneobunge la Laisamis, Kello amesema kuwa Serekali imeboresha utoaji wa chakula cha msaada kwa wakazi wa Laisamis kwa kuhakikisha kuwa kila eneo limepata chakula cha kutosha ili kuwasaidia wakazi ambao wamekumbwa na ukame jimboni.
Katibu huyu amedokeza kwamba serekali iliweza kuingilia kati masuala ya ugonjwa wa Kalaazar katika eneo la Loglogo kwa kuhakikisha kuwa wakazi wamepata lishe pamoja na hamasa ya kutosha
Kwa upande wake mwakilishi wadi wa Loiyangalani Daniel Emojo,amesema kwamba kwa mara ya kwanza wakazi wa kaunti kame nchini wameweza kushuhudia utendakazi wa idara ya ya maeneo kame na ustawi wa miji huku akimpongeza Rais William Ruto kwa uteuzi wa Kello Harsama kuwa katibu wa idara hiyo.
Kwenye ziara hiyo Kello aliweza kuambatana Leakono Bernard mwakilishi wadi wa Log Logo, James korie (MCA illeret), Emojo Musa (MCA Loiyangalani), Burcha Daniel (Laisamis), Golicha Ebise ambaye ni mwakilishi mteule pamoja na viongozi wengine kutoka kaunti ya Marsabit.