County Updates, Local Bulletins

SEREKALI YA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI DHABITI YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KALAAZAR.

Picha Hisani

Na JB Nateleng,

Idara ya afya katika kaunti ya Marsabit imedhibitisha kuwa Ugonjwa wa Kalaazar bado unazidi kuripotiwa hapa jimboni.

Kwa mujibu wa afisa wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Abdi Adan na ambaye ni meneja wa kituo cha kushughulikia maswala ya dharura Abdi Adan, ni kwamba Serekali ya kaunti ya Marsabit kwa ushirikiano na serekali kuu wamekita kambi katika eneo laLog Logo eneo bunge la Laisamis, na Shur eneo bunge la North horr ili kuendeleza utafiti wa ugonjwa wa Kalaazar huku visa vipya vikizidi kuripotiwa katika maeneo hayo.

Adan amesema kuwa bado wanaendeleza zoezi la kunyunyizia dawa makazi ya wenyeji wa maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo huku akitoa wito kwa wakazi wa Marsabit kuweza kuripoti kisa chochote cha ugonjwa huu haraka iwezekanavyo kwa idara husika.

Aidha Adan ameelezea kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit chini ya uongozi wa gavana Mohamud Ali inajisatiti kuhakikisha kuwa maeneo mengi yamepata zahanati na dawa za kutosha ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wote jimboni.

Hata hivyo afisa huyo wa afya ametoa wito kwa wakazi wa Marsabit kuweza kufuata maagizo yaliyotolewa na wizara ya afya ili kujikinga na baadhi ya magonjwa.

 

Subscribe to eNewsletter