Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na JB Nateleng,
Serekali ipo tayari kushirikiana na washikadau mbalimbali katika kuboresha na kuinua hadhi ya elimu katika kaunti ya Marsabit.
Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Elimu kaunti ya Marsabit Peter Magiri.
Kwenye hotuba yake iliyosomwa na mkurugenzi wa elimu kaunti ndogo ya North Horr Mamo Gutu ambaye alikuwa akimwakilisha Magiri wakati wa hafla ya kusherehekea siku ya elimu jimboni Marsabit ni kwamba serekali inajisatiti kutembelea shule zote jimboni kuhakikisha kwamba mazingira ambayo shule imejengwa ni bora na salama ili kuwalinda wanafunzi pamoja na walimu.
Magiri ameelezea kwamba idara ya elimu ipo tayari kupeana mawaidha kuhusu elimu kwa washikadau ambao wanataka kujenga shule ama kuboresha elimu hapa jimboni Marsabit.
Hata hivo Mapadri wanaosimamia parokia mbalimbali wametakiwa kushirikiana na maafisa wa elimu waliopo maeneo yao ili kuweza kupata maelezo zaidi kuhusu sheria za elimu.
Idara ya elimu pia imepongeza juhudi ya Kanisa katoliki katika kuboresha kiwango cha elimu katika jimbo la Marsabit, huku ikitoa wito kwa washikadau mbalimbali jimboni kuwekeza zaidi kwenye masuala ya elimu.