County Updates, Local Bulletins

SEKTA YA UVUVI JIMBONI MARSABIT YAPIGA HATUA HUKU ASILIMIA KUBWA YA WAKAZI WAKIKUMBATIA UVUVI.

Picha Hisani

Na JBNateleng

Tangu kuanzishwa kwa ugatuzi, sekta ya uvuvi jimboni Marsabit imeweza kupiga hatua huku asilimia kubwa ya wakazi wanaoishi karibu na ziwa Turkana wakikumbatia uvuvi.

Haya ni kwa mujibu wa afisa kutoka idara ya uvuvi kaunti ya Marsabit Sostine Nanjali.

Akizungumza na idhaa hii afisini mwake, Sostine ameeleza sekta ya uvuvi imekua jimboni kwa zaidi ya asilimia 100, akitaja uwekezaji wa serekali ya kaunti kwa ushirikiano na serekali kuu pamoja na mashirikia yasiyo ya kiserekali kuwa ni chanzo kikuu cha ukuaji huo.

Nanjali amesisitiza kuwa idara hiyo inazidi kuweka mikakati zaidi ili kuboresha na kuimarisha sekta ya uvuvi ambayo watu wengi wameanza kutegemea jimboni

Aidha Nanjali ametaja hatua ya Marekani kusitisha ufadhili wao kuathari sekta hiyo kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo afisa huyu amedokeza kwamba idara hiyo imeweza kutoa hamasa kwa wavuvi kujisimamia kwa kushirikiana na kuinua kitengo simamizi ya ziwa (BMUs) na kuwekeza zaidi ili kupata kipato cha kuwawezesha kununua bidhaa muhimu katika uvuvi.

Nanjali amewachangamoto wavuvi jimboni kuweza kufuata sheria za uvuvi ili kuepukana na migogoro ya mara kwa mara inayotokea kati ya maafisa wa serekali na wavuvi ziwani Turkana.

Subscribe to eNewsletter