County Updates, Local Bulletins

POLISI WANASA BANGI YA THAMANI YA SH.10M KATIKA ENEO LA ELEBOR SOLOLO.

Na Abdiaziz Yusuf,

Maafisa wa polisi wakishirikiana na maafisa wa akiba NPR wamefanikiwa kunasa bangi yenye dhamana ya shilingi milioni 10.5 katika eneo la Elebor eneobunge la Sololo  kaunti ya Marsabit.

Akithibitisha tukio hilo OCPD wa Sololo Joseph Nthiga amesema kuwa bangi hiyo ilikuwa imefichwa ndani ya gari aina ya Land Cruiser saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Aidha Nthiga amesema kuwa wamefanikiwa kumkamata dereva wa gari hilo baada ya yeye kupata jereha kidogo mguuni na anaendelea kupata matibabu katika hosipitali ya Sololo chini ya ulinzi wa polisi.

Hata hivyo amepongeza ushirikiano wa mafisa wa polisi wa akiba na ametoa wito kwa wananchi wote  kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kukomesha biashara hiyo haramu.

Subscribe to eNewsletter