Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Caroline Waforo,
Uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa ambapo afisa mmoja wa polisi amejitia kitanzi katika kaunti ndogo ya Turbi kaunti ya Marsabit hapo jana Jumapili.
Kulingana na naibu kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Turbi Bubisa Daniel Parmwat mwili wa afisa huyo ulipatikana ukiwa umeninginia kwenye mti, mita chache kutoka nyumbani mwake.
Naibu Kamanda Parmwat amesema kuwa wanaendeleza uchunguzi ili kubaini kiini cha kisa hicho na sababu iliyopelekea afisa huyo na ambaye alikuwa na historia ya kubugua pombe kujitoa uhai.
Na kutokana na kuongezeka kwa visa vya maafisa kujitia kitanzi, Parmwat amewataka maafisa hawa kutafuta misaada wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha huku pia akiwataka kuasi utumizi wa pombe na dawa za kulevya.
Itakumbukwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita afisa wa polisi aliyekuwa akihudumu katika kaunti hii ya Marsabit alijitia kitanzi baada ya kuwaua watoto wake wawili na mtoto mwengine wa shemeji yake kwa kuwapa sumu katika eneo la Kakdhimu huko Rachuonyo, kaunti ya Homa Bay.
Afisa huyo aliwacha barua iliyoleza masaibu aliyoyapitia, ya kifamilia na pia ya kikazi.