County Updates, Local Bulletins

POLISI MOITE, LOIYANGALANI MARSABIT WAFANIKIWA KUREJESHA NGAMIA 8 KATI YA 16 WALIOBIWA WIKI JANA.

(Loiyangalani)

Na Caroline Waforo

Maafisa wa polisi katika eneo la Moite wadi ya Loiyangalani kufikia wamefanikiwa kurejesha ngamia wanane waliokuwa wameibiwa ya Alhamisi iliyopita na wezi wa mifugo.

Akithibitisha kisa hicho naibu kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Loiyangalani Nicholas Mutua, ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, amesema kuwa wahalifu waliiba mifugo hao waliokuwa wakichungwa na watoto.

Anasema kuwa kurejeshwa kwa ngamia hao 8 kati ya 16 waliokuwa wameibiwa imefanikishwa kwa ushirikiano na naibu kamanda wa kaunti ndogo ya North Horr

Mutua ameendelea kutoa tahadhari kwa wazazi dhidi ya kuwapa watoto wadogo majukumu ya kulisha mifugo haswa maeneo ya mbali hususan msimu huu wa likizo ndefu ya mwezi Aprili akisema kuwa pia inahataraisha maisha yao.

Mutua amesema kuwa wanaendelea kuwasaka ngamia waliosalia huku akiwahakikishia wakaazi wa eneo hilo usalama wa kutosha akisema kuwa wameimarisha doria katika kaunti ndogo ya Loiyangalani.

Subscribe to eNewsletter