Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng,
Ili kuepukana na ugonjwa wa kisukari ni sharti tubadili mtindo wa maisha kwa kufanya mazoezi kila mara.
Haya ni kwa mujibu wa afisa anayeshughulika ugonjwa wa kisukari kisukari katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Steve Sereti.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya Kipekee, Sereti ameelezea kwamba ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa ambao unaweza epukika iwapo tu watu watabadili miendendo ya uvivu na badala yake kuendeleza mienendo ambayo ni ya mazoezi na kula chakula kinachofaaa.
Sereti ameelezea kwamba ugonjwa wa kisukari huja na madhara mengi katika mwili hivyo kuwarai wakazi kuenda hospitalini ili kujua hali yao ya afya.
Aidha Sereti ameelezea kwamba watoto wadogo pia wapo kwenye hali ya kupata aina ya kwanza ya ugonjwa huu (Diabetes type 1) huku wataalam wa afya wakizidi kufanya uchunguzi wa kubaini chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watoto wachanga.
Vilevile Sereti ametaja matumizi ya mafuta ya kupikia kupita kiasi kuwa kunasambaratisha jinsi ambavyo viungo vya mwili vinapambana na maradhi hivyo kuhatarisha binadamu kupata ugonjwa wa kisukari na hata magonjwa mengine.
Mtaalam huyu ameta kwenda haja ndogo sana na kuhisi kiu kila mara kama dalili za ugonjwa wa Kisukari huku akiwataka wale ambao watagunduliwa kuwa na ugonjwa huu kuanza matibabu mapema.
Pia ameitaka serekali k kuwekeza katika kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na kuwasaidia wale ambao wanaishi na ugonjwa wa kisukari kwa kuwapunguzia gharama ya Matibabu.