County Updates, Local Bulletins

MWENYEKITI WA HAZINA ZA CDF ENEO BUNGE LA SAKU AELEZA KUHUSU UZINDUZI WA FEDHA ZA CDF

NA Hendry Khoyan

Wakaazi wa eneo bunge la Saku, hususan wazazi na walezi wa wanafunzi shuleni, wana kila sababu ya kufurahia. Mwenyekiti wa Hazina za CDF eneo bunge la Saku, Guyo Bonaya, ametangaza rasmi kuwa fedha za CDF zitazinduliwa mara baada ya kukamilika kwa mpangilio kati ya ofisi hiyo na Mbunge wa Saku, Ali Dido Raso.

Guyo Bonaya amesema kuwa kati ya Zaidi ya shilingi milioni 40 zinazotarajiwa, shilingi milioni 20 tayari zimepokelewa.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa fedha hizo hazitaweza kutolewa hadi kiasi chote kitakapopatikana, kwani milioni 21 ni chache kulingana na idadi ya wanafunzi wanaotegemea msaada huo.

Aidha, Bonaya ametoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha mpango huu unafanikiwa kwa manufaa ya wanafunzi wote.

Guyo amewahakikishia wanafunzi ambao wanahofia kufukuzwa kuoka shuleni na ambao ni wapokeaji wa fedha za CDF kuwa, hivi karibuni, barua ya kujiweka wazi (commitment letter) itatumwa kwa Idara ya Fedha kwa shule hizo.

Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi hao hawataathirika na kukosa kufanya mitihani yao kutokana na changamoto za kifedha.

Guyo amesisitiza umuhimu wa elimu na haki ya wanafunzi wote kupata fursa ya kujifunza bila vikwazo.

Amesisitiza kuwa mwanafunzi hawezi kulipiwa karo yote na kwamba wazazi wanapaswa kuchangia kwa kiwango fulani.

Guyo ametoa wito kwa wanafunzi kutoa malalamiko yao mapema na kwa njia sahihi.

Ameonya dhidi ya kulalamika kupitia mitandao ya kijamii, na badala yake amesisitiza umuhimu wa kufikisha malalamiko yao kwa viongozi wao ili waweze kupata suluhisho kwa wakati.

Subscribe to eNewsletter