County Updates, Local Bulletins

MWANAUME MOJA ASHTAKIWA KWA KUMLAWITI WA MTOTO WA MIAKA 4 MARSABIT

Na Mwandishi wetu

Mwanaume moja ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa makosa mawili ikiwemo ulawiti wa mtoto wa miaka 4.

Mahakama imearifiwa kuwa tarehe 7 mwezi Machi mwaka 2025 katika eneo la Kubi Kalo lililoko katika kaunti ndogo ya Marsabit Central kaunti ya Marsabit mshukiwa Kana Barako alimtendea kitendo hicho cha unyama mtoto huyo.

Katika kosa la pili mshukiwa huyo ameshtakiwa kwa mshuka visivyo mtoto huyo.

Mshukiwa alikamatwa tarehe 11 mwezi Machi na kufikishwa mahakamani tarehe 13 mwezi uo huo mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome

Mshukiwa alikana mashtaka yote mawili na kudai kuwa ana umri wa miaka 16.

Mahakama iliamuri mshukiwa kufanyiwa uchunguzi hospitalini ili kubaini umri wake ambapo ilibainika kuwa ana kati ya umri wa miaka I8-21.

Mahakama ilimpa mshukiwa huyo bondi ya shilingi 200,000 au pesa taslimu shilingi 100,000

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 14 na kusikilizwa tarehe 29 mwezi Aprili mwaka 2025.

Subscribe to eNewsletter