County Updates, Local Bulletins

MWANAMME ALIYEMNAJISI MSICHANA WA MIAKA SABA KATIKA ENEO LA SONGA, MARSABIT, AKAMATWA.

Picha Hisani

Na Isaac Waihenya,

Hatimaye mwanamme aliyemnajisi msichana wa miaka saba katika eneo la Songa, eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit ametiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa naibu chifu wa eneo la Songa Luka Lekipayan, ni kuwa mwaname huyo mwenye umri wa makamu ametiwa mbaroni katika eneo la Hulahula alikokuwa amejificha na kisha kusafirishwa hadi katika kituo cha polisi cha Central anakoendelea kuizuiliwa.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu chifu Lekipayan amepongeza waliotoa ripoti muhimu kwa asasi za usalama ambazo zimesaidia katika kuhakikisha kwamba mhalifu huyo amekamatwa.

Aidha chifu Lekipayan ametoa wito kwa wazazi kuwachunga wanao haswa msimu huu wa likizo ndefu ya mwezi Aprili ili kuwaepusha na madhara kama hayo.

Vilevile amewaonya wale wanaoendeleza uovu huo katika eneo hilo, kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Haya yanajiri huku washikadau mbalimbali katika sekta ya elimu na idara ya watoto wakizidi kukashifu visa vya unajisi ambao vimetajwa kuongezeka katika maeneo mbalimbali hapa jimboni, huku wakitoa wito kwa asasi za kuisalama kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaotekeleza uovu huo.

Subscribe to eNewsletter