Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Joseph Muchai,
Mwakilisha wadi wa Loiyangalani Daniel Emojo Musa ameelezea masikitiko yake kuhusu kutangazwa upya kwa nafasi ya naibu chifu katika kata ya Loiyangalani. Akizungumza na wanahabari mjini Marsabit Emojo amesema kuwa shughuli hiyo iliingiliwa na viongozi wenye ushawishi kwani kulingana naye shughuli ya kupigwa msasa kwa wawaniaji wa nafasi hiyo ilikamilika ila baada ya muda nafasi hiyo ikatangazwa tena kuwa ipo wazi.
Kulingana na Emojo jamii ya Turkana imepuuzwa na kutelekezwa katika nafasi hiyo huku akitaja kwamba anahisi kuwa jamii hiyo ambayo ina idadi kubwa ya watu katika eneo hilo haijapewa kipaumbele.
Aidha Emojo amelalamika kuwa eneo hilo limesalia nyuma kwani kwa kipindi kirefu hawajakuwa na uwakilishi na hivyo kuwanyima fursa ya kufurahia huduma muhimu za serikali huku akitoa wito kwa washikadau katika mchakato wa kuwapiga msasa wawaniaji wapya kufanya jukumu lao kwa uadilifu.
Hata hivyo mwakilishi wadi huyo anahisi kwamba shughuli hiyo itakuwa huru na wazi kwani baadhi ya walioingilia kati zoezi la awali hawamo tena.