Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Marsabit Bi. Naomi Jillo Wako amewakosoa wale ambao wanaendeleza kampeni ya Ruto Must Go akiwataja kama maadui wa maendeleo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za kujenga kanisa katika shule ya wasichana ya Moi Girls hapa mjini Marsabit, Naomi ametaja kwamba serekali ya Kenya Kwanza haita-tatizwa na upande wa upinzani unaoendeleza ajenda hiyo na badala yake itaangazia kuendeleza ajenda ya maendeleo kwa wote.
Aidha Bi. Naomi amewataka wanaendeleza kampeni hiyo kuwa tayari kwa rais Wiliam Ruto kuendeleza uongozi wake na kuhudumu kwa mihula miwili.
Naomi vilevile ameurai upinzani kumpa muda rais ili aweze kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.