Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Samuel Kosgei
Maafisa wa polisi katika eneo la Loiyangalani, kaunti hii ya Marsabit wamemuokoa msichana mdogo wa miaka 12 kutoka kwa dhulma ya ndoa ya utotoni.
Kulingana na ripoti iliyoandikishwa kwenye kituo cha polisi cha Loiyangalani ni kuwa maafisa wa polisi walivamia kijiji cha Yomo eneo ambalo harusi ya kitamaduni ilikuwa ikifanyika jana Jumatano.
Inatajwa kuwa msichana huyo mwenye miaka 12, alikuwa akifungishwa ndoa kwa mshukiwa Loroo Aesekon 30, baada ya mahari ya ngamia watano, mbuzi 100 na punda wanne kulipwa kama mahari na wazazi wa mshukiwa ambao ni Lochomin Ekeno na Asimit Epong.
Mshukiwa Aesekon, wazazi wake na wazazi wa msichana mwathiriwa wote walikamatwa na polisi na kufikisha kituo cha polisi cha Loiyangalani kuandikisha kuhojiwa Zaidi.
Maafisa wa polisi idara ya DCI Loiyangalani wanafuatilia kisa hicho.