County Updates, Local Bulletins

MBUNGE WA LAISAMIS JOSEPH LEKUTON AITAKA KAMPUNI YA KENGEN KUWA NA UWAZI INAPOANZISHA MRADI WA UMEME LOIYANGALANI/MT KULAL

Hon Joseph Lekuton – MP Laisamis

Na Samuel Kosgei

MBUNGE wa Laisamis Joseph Lekuton ameitaka kamati ya Kawi katika bunge la kitaifa kuelezea kuhusiana na mpango wa kampuni ya KenGen kuanzisha na mtambo mwingine wa kuzalisha nguvu za umeme kupitia upepo katika wadi ya Loiyangalani, Laisamis kaunti ya Marsabit.

Akizungumza katika bunge la kitaifa Lekuton aliambia bunge kuwa kampuni ya KenGen haijizangatia suala la uwazi na uwajibikaji inapopanga kuanzisha mradi huo wa mabilioni ya pesa mwaka ujao.

Lekuton anasema kuwa licha kampuni hiyo kufanya vikao vya kuhamasisha umma wakaazi wa wa Mt. Kulal, Loiyangalani na Laisamis kwa ujumla hawana uwazi kamili wa mradi huo haswa kwenye suala la kubadilishwa kwa ujenzi wa barabara unaoelekea katika eneo la mradi huo.

Amesema kuwa wakaazi wa eneo hilo wangetaka kufahamu miradi itakayowafaa kwani wana haki ya kujulishwa na kampuni yenyewe huku wakitaka mradi wa barabara kujengwa ndani ya eneobunge la Laisamis kutokana na eeno hilo kuzalisha rasilmali hiyo ya upepo.

Masuala mengine aliyotaka kamati kawi kueleza ni pamoja na ukubwa na hekari za ardhi itakazotumika kuanzishwa kwa mradi huo kati ya nyingine

Subscribe to eNewsletter