Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Samuel Kosgei
ZAIDI ya vyama vya ushirika 40 kutoka Moyale kaunti hii ya Marsabit yameshirikiana kuunda muungano mmoja mkubwa ili kushughukulia maslahi yao katika harakati za kuchimba migodi eneo la Hillo.
Kulingana na mwenyekiti mpya wa muungano huo wa wachimba migodi Moyale Rashid Karayu ni kuwa kuanzishwa kwa muungano huo ni kigezo kimoja cha migodi za dhahabu eneo la Hillo kuweza kufungiliwa na serikali.
Anasema kupitia kufanya kazi pamoja itakuwa rahisi kwa serikali kuwakubalia kufungua migodi hizo.
Karayu ambaye amechaguliwa kwenye uchaguzi uliofanyika siku ya Alhamisi kuwa mwenyekiti amesema jamii zote za eneo hilo zimehusishwa na wote wameridhika kinyume na iliyokuwa miezi kadhaa iliyopita ambapo jamii moja ilijiondoa.
Amepuuzilia mbali uvumi kuwa vyama vya ushirika vinaenda eneo hilo kuwafurusha wachimba migodi walio katika machimbo hayo. Hata hivyo amewataka wale ambao hawajajiunga na vyama vya wachimba migodi kujiunga navyo kwa haraka.
Uchaguzi huo wa viongozi wa Muungano wa Moyale Artisanal Union unajiri siku chache baada ya serikali kupitia waziri wa usalama kipchumba murkomen kuahidi kufunguliwa kwa migodi hiyo hivi karibuni.