KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Samuel Kosgei
Maafisa wa uchaguzi wa chama tawala cha UDA kimepongeza wagombeaji wa viti mbali mbali kwa kuonesha utulivu na ukomavu wao wakati wa zoezi la uchaguzi wa mashinani uliofanyika wikendi iliyopita kaunti hii ya Marsabit.
Maafisa hao wa kuendesha uchaguzi mashinani wakizungumza mjini Marsabit baada ya kuwapa vyeti washindi wa uchaguzi huo wamewataka wote walioshinda kuhudumia wanachama wote wa chama kwa njia ya heshima na uwazi bila kubagua yeyote huku pia wakitakiwa kuvumisha umaarufu wa chama hicho mashinani.
Veronica Chebet ni naibu mwenyekiti wa bodi ya kitaifa ya uchaguzi wa chama cha UDA.
Viongozi hao wa uchaguzi pia wamesema kuwa malalamishi yote yaliyowasilishwa mbele yao yameshughulikiwa ndani ya chama huku akisema kura hizo zilipigwa kwa njia digitali ili kuepusha visa vya udanganyifu.
Mmoja wa wagombeaji Bonaya Doti, amesema kuwa aliridhishwa na zoezi la uchaguzi huo kwani kulingana naye ulikuwa uchaguzi wa haki na usawa.
Kulingana na afisa Chebet Zoezi la uchaguzi wa chama hicho kilifanyika katika vituo 195 kote jimboni huku nyadhifa 20 zikijazwa na wanaume, wanawake, vijana, watu wanaoishi kwa ulemavu kati ya nafasi nyingine.