Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Joseph Muchai,
Siku moja baada ya Rais William Ruto kushambuliwa kwa kiatu katika kaunti ya Migori, viongozi wa kidini wametoa hisia mseto kuhusiana na swala hilo.
Wa hivi punde kutoa kauli yake ni mchungaji wa kanisa la KAG Marsabit Reverend Joseph Mwenda.
Akiongea na Shajara ya Radio Jangwani mchungaji Mwenda amekashifu kitendo hicho akisema kuwa hilo sio suluhu la matatizo yanayowakumba wananchi.
Aidha mchungaji huyo amewataka Wakenya kutumia njia mwafaka za kutatua mizozo kwani nchi ya Kenya ina katiba ambayo inashughulikia maswala kisheria.
Wakati uo huo mchungaji Mwenda ametoa wito kwa wananchi kumpa rais nafasi ya kufanya kazi kikatiba na kuombea nchi na rais badala ya kutumia hasira kama silaha.