County Updates, Local Bulletins, Sport Bulletins

KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.

Na Isaac Waihenya

Kosh United kutoka Kituruni ndio mabingwa wa taji la NAPO Conservations Cup mwaka wa 2025.

Kosh walitwa ubingwa baada ya kuilaza timu ya Loitorio FC kwa jumla ya magoli mawili kwa nunge.

Magoli ya Kosh United yalitiwa kimywani na wachezai Balang Modrich kunako dakika ya pili kabla ya mchezaji Ken Mbappe kutia kimyani goli la pili kunako dakika ya 18.

Juhudi za Loitorio FC kurejea katika mechi hiyo hazikuifua dafu baada ya mlinda lango wa timu ya Kosh United kuokoa mashutii kadhaa.

Akizungumza baada ya ushindi huo nahodha wa timu ya Kosh United Isaac Komboi ametaja kufurahia ushindi huo huku akiwapongeza wachezaji wenzake kwa kuonyesha ukakamamu katika makala ya mwaka huu.

Aidha Komboi ameweka wazi kama washindi wataendeleza majukumu ya kutunza na kuhifadhi mazingiri kama yalivyo malengo ya shirika la Nature and People as One (NAPO).

Katika upande wa akinadada timu ya Kulapesa FC kutoka eneo la Burkacha ndio mabingwa wa makala ya mwaka huu ya NAPO Conservations Cup baada ya kuilaza timu ya akinadada ya Rising Stars kutoka Karare mjini kwa jumla ya magoli 5-4 kupitia matuta ya penalti.

Mechi hiyo iliishia sare ya goli moja kwa moja katika muda wa dakika tisini na kulazimu mshindi kuitafutwa kupitia matuta ya penelti.

Kulapesa walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kupitia mcheza Ntipik Leruk kunako dakika ya 19 katika kipindi cha kwanza kabla ya mchezi Lulu Esimonte kusawazisha kunako dakika ya 63 kipindi cha pili.

Kwenye mkao na vyombo vya habari baada ya ushindi huo nahodha wa Kulapesa FC, Sofina Loimanga, ametaja kwamba ushindi huo umetokana na ushirikiano kati yao huku alishukuru shirika la NAPO kwa kuwahusisha wasichana katika zoezi la kabumbu na pia kuhifadhi mazingira.

Kauli yake ilishabikiwa na meneja wa kikosi hicho Samwel Nure ambaye pia aliitaja kama hatua kubwa kuwahusisha wasichana katika michuano hiyo na pia uboreshaji wa mazingira.

Kwa upande mkurugenzi mkuu wa shirika la NAPO Adrien Loitoro amepongeza vilabu vyote vilivyoshiriki katika makala hayo ya mwaka wa 2025, huku akiyataja kama yaliyofana zaidi kutokana na kujuisha timu za akinadada.

Ameahidi kuwa shirika hilo litazidi kuboresha michuano hiyo na hata kuzidisha juhudi zao katika kutunza na kuhifadhi mazingira huku akifichua kuwa mwaka huu wa 2025 pekee shirika hilo limepanda, kuhifadhi na hata kulinda zaidi ya miti 7,000.

Makala ya mwaka huu yalijuimuisha timu 34 ambapo timu 4 zilikuwa za akina dada huku 30 zikiwa za wavulana, hii ikiwa na mara ya kwanza wanadada kushiriki katika michuano hiyo tangu kuasisiwa kwake mwaka wa 2023.

Vilabu vyote viivyoshiriki vimetunukiwa jezi na mpira mmoja wa miguu huku washindi wa taji la msimu huu upande wa wavulana Kosh United wakitia kibidoni shilingi 15,000.

Nambari mbili Loitorio FC walitunukiwa shilingi 7,500 huku timu ya Maaram FC ikienda nyumbani na shilingi 10,000 baada ya kuzawadiwa kama timu iliyofanya bora katika kutunza mazingira mwaka huu.

Kwa upande wa kinadada mabingwa wa mwaka huu Kulapesa FC walikwenda nyumbani na shilingi 5,000 huku Rising Stars waliokamilisha katika nafasi ya pili wakitunukiwa shilingi 2,500.

Subscribe to eNewsletter