County Updates, Local Bulletins

IDARA YA WATOTO MARSABIT, YAKEMEA ONGEZEKO LA VISA VYA UNAJISI.

Na Isaac Waihenya,

Idara ya watoto katika kaunti ya Marsabit imekemea visa vya unajisi ambavyo vimetajwa kuongezeka katika maeneo kadhaa kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa afisa wa idara ya watoto katika kaunti ya Marsabit Mukanzi Leakey ni kuwa baadhi ya visa hivi vinachangiwa na baadhi ya jamii kuendeleza tamaduni ambazo zimepitwa na muda.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake Mukanzi amesema kwamba idara hiyo inazidi kufuatilia visa hivyo ili kuhakikisha kwamba waadhiriwa wanapata haki.

Aidha afisa huyu wa watoto amewataka wazazi kushirikiana na idara hiyo ili kuhakikisha kwamba watoto wote wako salama msimu huu wa likizo na waweze kujerejea shuleni wakati shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa pili.

Vilevile Mukanzi amewarai wazazi kutatua mizozo ya ndoa kwa namna na ambayo haitadhiri watoto haswa kisaikolojia.

Subscribe to eNewsletter