Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
NA Samuel Kosgei
Idara ya Utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Marsabit imetabiri kuwa kwa siku saba zijazo kuanzia leo Jumanne tarehe 8 hadi 14 Aprili 2025 kutakuwepo na ongezeko kwa kiasi kikubwa cha mvua na usambazaji wake katika maeneo mengi ya Kaunti ya Marsabit ikilinganishwa na wiki iliyopita.
Mvua nyepesi hadi ya wastani asubuhi pamoja na manyunyu ya mchana na usiku inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi ya Kaskazini na Kaskazini-Mashariki mwa Kaunti wakati wa kipindi cha utabiri.
Kulingana na mkurugenzi wa idara hiyo kaunti ya Marsabit John Nguyo Usambazaji wa mvua unatarajiwa kuongezeka ikilinganishwa na kipindi cha awali cha utabiri (tarehe 1 hadi 7 Aprili 2025).
Upepo wa kasi pia unatarajiwa katika maeneo kadhaa ya Kaunti.
Kutokana na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya kanda hii ya mashariki ya juu, Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya imetoa onyo la uwezekano wa mafuriko katika maeneo ya mabonde ya chini, mito ya msimu. Wananchi kote nchini wameonywa wasijaribu kuvuka barabara, madaraja, au mito iliyojaa maji ya mafuriko.