KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Huenda kero la ukosefu wa maji katika eneo la Boke wadi ya Maikona kaunti ya Marsabit likapata suluhu baada ya idara ya maji kaunti ya Marsabit kuahidi kushugulikia kisima cha Log Lokho katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa maswala ya teknolojia katika idara ya maji kaunti ya Marsabit Shanke Stephen Katelo, ni kuwa idara ya maji imeweka mikakati kabambe kuhakikisha kwamba tatizo hilo ambalo limedumu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa linatatuliwa.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Katelo amebainisha kwamba wataalam katika idara hiyo watazuru kisima hicho ili kupata suluhu kuhusiana na iwapo ni kinaweza rekebishwa au ni hatua zipi zingine zitakazochukuliwa.
Katelo amewataka wakaazi wa eneo hilo kuwa na subira idara hiyo inapoendeleza juhudi za kuhakikisha kwamba wanapata maji.