Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Mwandishi Wetu
Idara ya ufugaji kaunti ya Marsabit ingali kupokea ripoti ya matokeo kuhusu ugonjwa ulioagamiza ngamia wapatao ishirini katika eneo la Huri Hills eneobunge la North Horr mwezi jana.
Afisa wa chanjo ya mifugo katika eneo hilo, Tuna Dabaso amesema kuwa sampuli ya wanyama hao waliokufa ilipelekwa katika maabara ya mifugo eneo la Kabete ili kufahamu sababu kamili ya vifo hivyo vya ngamia.
Dabaso ameambia shajara kuwa maabara ya mifugo iliyo hapa Marsabit haina uwezo wa kutambua sababu mwafaka ya vifo hivyo vilivyofanyika mapema mwezi wa tatu.
Hata hivyo amesema kuwa ngamia hao kwa sasa hawakufi tena na maradhi hayo yalidhibitiwa.
Kulingana na Mamlaka ya kukabili majanga na athari za ukame kaunti ya Marsabit NDMA kwenye ripoti yake ya mwezi uliopita ilidai kuwa huenda maafa ya ngamia hao ilisababishwa na maambukizi kutoka kwa kupe.
Wakati huo huo ripoti yao ya mwezi wa tatu unaonesha kuwa kwa sasa, aina nyingi ya mifugo inaonyesha hali nzuri ya mwili.
Uzalishaji wa maziwa pia unaoneka upo juu kidogo ya kiwango cha kawaida. Wafugaji pia hawakuhama kwa sana kusaka lishe na maji.