County Updates, Local Bulletins

DCI YATAKIWA KUCHUNGUZA WIZI WA VIRUTUBISHI VYA CHAKULA KATIKA HOSPITALI ZA UMMA.

Na Mwandishi Wetu

Idara ya uchunguzi DCI kaunti ya Marsabit imetakiwa kuchunguza madai kuwa virutubishi vya chakula vinaibwa kutoka katika vituo vya afya vya serikali na kuuzwa kwa wafanyabiashara wasio waaminifu. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Moyale na Loiyangalani.

Kamati ya usalama hapa Marsabit ikiongozwa na kamishna wa kaunti, maafisa wa usalama kaunti ndogo ya Loiyangalani, timu ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP, serikali ya kaunti kati ya wengine wamebainisha kuwa virutubishi ya vyakula vilivyolenga kuwasaidia wakaazi hospitalini vinaibiwa mara kwa mara.

Kama njia moja ya kusitisha hulka hiyo ya wizi wa vyakula idara ya usalama imetakiwa kufanya uchunguzi na kuwatia mbaroni wahalifu wanaohusishwa.

Aidha maafisa wawili wa NPR wametakiwa kulinda kontena katika zahanati ya Loiyangalani pamoja na walinzi waliopo ili kuzuia wizi huo.

Machifu pia katika maeneo husika wametakiwa kuandaa orodha ya wahalifu wote na wachunguzwe huku pia Jamii ikitakiwa kufahamu kuhusu athari za wizi wa chakula.

Subscribe to eNewsletter