KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na JB Nateleng,
Wakazi wa Marsabit wameshauriwa kuhakikisha kuwa wametunza na kunywa maji safi kwa ajili ya kujikinga na maradhi yatokanayo na matumizi ya maji chafu.
Kwa mujibu wa afisa wa afya ya umma na ambaye pia ni mshirikishi wa idara ya WASH jimboni Marsabit Roba Wario aliyezungumza na idhaa hii kwa njia ya kipkee, ameelezea kuwa asilimia 60 ya wafugaji jimboni hutumia maji ya silanga ambayo kulingana na uchunguzi si safi na huenda yakaathiri afya yao.
Wario amewataka wafugaji kutumia dawa za kusafisha maji ambazo zinapatikana katika zahanati zote mashinani huku akiwashauri wakazi kutumia vyoo ili kuepukana na uchafuzi wa maji wakati wa huu wa msimu wa mvua.
Kadhalika Roba amewataka wakazi kuhakikisha kuwa mitungi ya kutekea maji ni safi na maji hayo yachemshwe kabla ya kuyakunywa.