County Updates, Local Bulletins

CHAMA CHA WALIMU KNUT CHAITAKA BARAZA LA MITIHANI KNEC KUONDOLEA WALIMU MALIPO YA MAFUNZO YA CBC.

Picha Hisani

Na Samuel Kosgei

Chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za msingi KNUT tawi la Marsabit kimesema kuwa wizara ya elimu inafaa kutoa mafunzo ya walimu wanaosomesha mfumo wa CBC bila malipo yoyote.

Akizungumza na kituo hiki katibu wa chama hicho cha KNUT tawi la Marsabit Rosemary Talaso amesema kuwa mafunzo hayo kwa walimu CBC ina umuhimu mkubwa japo itakuwa vigumu kwa walimu kuhudhuria kutokana na malipo yanayotakiwa kila mwalimu alipie.

Hata hivyo mwalimu Rosemary amependekezea idara ya elimu nchini kupeleka mafunzo hayo ya CBC katika kaunti mbalimbali nchini ili kupunguza gharama ambayo walimu wangetumia kufanikisha mafunzo hayo badala ya kusafiriki hadi jiji la Nairobi.

Kwenye taarifa yake hii leo baraza la kusahihisha mitihani nchini KNEC imealika walimu nchini na wakufunzi kuomba nafasi ya kwenda kupewa mafunzo ya CBC na namna ya kuangazia mitihani ya kutathmini wanafunzi.

Subscribe to eNewsletter