County Updates, Local Bulletins

BUNGE LA SENATE LATAKIWA KUHARAKISHA KUTATUA MGOGORO UNAOHUSU ARDHI YA MAKABURI HAPA JIMBONI MARSABIT.

Na Isaac Waihenya,

Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi nchini (NLC) Qabale Tache Elema, amelitaka bunge la Senate kuharakisha kutatua mgogoro unaohusu ardhi ya makaburi hapa jimboni Marsabit.

Akizungumza na vyombo vya habari Bi. Qabale ametaja kwamba hata licha ya mahakama kushikilia uamuzi wa tume hiyo wa kutupilia mbali hatimiliki za waliokuwa wameinyakua ardhi hiyo, bado swala hilo halijaidhinishwa rasmi.

Aidha Qabale ametoa wito kwa bunge la Senate kuharakisha mchakato huo ili kuhakikisha kwamba swala hilo linatuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile ameahidi kuwa tume ya ardhi inaendeleza mikakati kabambe kuhakikisha kuwa inasuluhisha maswala ya mizozo ya ardhi humu nchini.

 

Subscribe to eNewsletter