County Updates, Local Bulletins

BUNGE LA MARSABIT LAHOJI WANACHAMA WA JOPO LA KUTEUA BODI YA UAJIRI WA KAUNTI.

Bunge la Marsabit

Na Samuel Kosgei

Bunge la kaunti ya Marsabit hii leo limepiga msasa na kulihoji jopo la watu watano litakaochagua wanachama wa bodi ya uajiri ya kaunti Marsabit (Marsabit Public Service Board).

Jopo hilo la uteuzi lilifika mbele ya kamati ya upigaji msasa ya bunge leo jumanne likiongozwa na spika Edin Wario Dida.

Waliopigwa msasa ni pamoja na David Dida Wario (anayependekezwa kuwa Mwenyekiti), Sabdio Roba Okile anayewakilisha sekta ya kibinafsi, John Galimogle mwakilishi wa taasisi ya wahasibu nchini ICPAK, Abdilatif Jarso anayewakilisha mawakili na Mariam Challa anayewakilisha muungano wa wafanyakazi.

Kamati ya bunge ya upigaji msasa sasa inatarajiwa kuchambua ripoti yake kabla ya kuwasilisha ripoti hiyo bungeni na ili kuidhinishwa na wawakilishi wadi wote.

Subscribe to eNewsletter