Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Sebalua Moses
Kutokana na mvua iliyonyesha hivi maajuzi wakaazi wa eneo la Korr kaunti hii ya Marsabit wamelalamikia barabara mbovu ya kuelekea huko kutoka Loglogo huku wakisema kuwa shughuli za usafiri zimeathirika tangu jana Jumanne.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kupitia njia ya simu, chifu Job Edimole kwa niaba ya wakaazi amesema kuwa barabara hiyo imekua katika hali mbovu hata kabla ya mvua kunyesha na hivyo mvua iliiharibu zaidi.
Vile Vile chifu Edimole ameiomba serikali iweze kuwasaidia katika ujenzi wa barabara hiyo muhimu ili waweze kuendeleza shughuli zao kawaida .