County Updates, Local Bulletins

BAADHI YA WAKAAZI WA MARSABIT WAPINGA HATUA YA MKUU WA POLISI KUHUTUBU KWENYE ZIARA YA RAIS.

Na Kosgei Samuel

Hatua ya Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja kuonekana kwenye msafara wa rais William Ruto kaunti ya Nyeri maajuzi katika ziara yake ya mlima Kenya inazidi kukosolewa vikali katika baadhi ya maeneo nchini.

Wakaazi wa Marsabit waliozungumza nasi wametaja hatua hiyo kuwa isiyo bora kwani inaonekana wazi kuwa inspekta Jenerali amechukua msimamo suala lisilofaa kulingana na katiba.

Baadhi ya wanaopinga hatua hiyo wamemtaka inspekta jenerali kufuata katiba na kulinda wakenya wote bila kuchukua msimamo wa kisiasa.

Hata hivyo baadhi wakiongozwa na Kinyua Mugo wamesema kuwa uwepo wa mkuu wa polisi kwenye ziara ya rais ulikuwa muhimu ili kuogopesha wahalifu na makundi yaliyokusudia kuvuruga mikutano ya rais.

Wakati uo huo wakaazi hao kutoka mjini Marsabit wamesema kuwa hawaoni haja ya Tume ya mgao wa mapato (CRA) kuongezea jimbo hili pesa Sh. 1.5bn katika mwaka mpya wa kifedha wakidai kuwa hawaoni kazi iliyofanywa na Zaidi ya shilingi bilioni 8 ambazo Marsabit hupokezwa kila mwaka wa kifedha.

Subscribe to eNewsletter