Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Asilimia 99 ya wanafunzi katika kaunti ya Marsabit wamerejea shuleni kwa muhula wa pili.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa ubora wa elimu kauti ya Marsabit Murmas Wanyama.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake, Wanyama amesema kuwa kwa sasa wanafunzi wanaendelea na elimu huku walimu wote wakiwa tayari wameripoti shuleni.
Aidha Wanyama ameweka wazi kuwa mikakati yote imewekwa ili kuhakikaisha kwamba masomo yanaendelea bila kutatizika.
Wanyama amesema kuwa mvua inayoshuhudiwa kwa sasa haija-adhiri masomo kwa vyovyote vile na pia hakuna uharibifu wowote katika shule mbalimbali hapa jimboni.
Hata hivyo afisa huyo wa ubora wa elimu hapa jimboni amewataka wazazi ambao hawajawapeleka wanao shuleni kufanya vile kwani ni haki ya kila mwanafunzi kupata elimu nchini.