Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng,
Asilimia 95 ya watu hupata ugumu wa kutambua iwapo wanaugua ugonjwa wa shinikizo la damu (Hypertension) kwani ugonjwa huu huchukua muda kuonyesha dalili ama wakati mwingine kukosa kuwa na dalili zozote.
Haya yamewekwa wazi na Daktari Steve Sereti ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee ni kwamba njia pekee, Sereti amesema kuwa wananchi wanaweza kujua iwapo wanaugua ugonjwa wa shinikizo la damu kupitia kufanyiwa vipimo na mtaalam wa afya hukua akitaja kwamba ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa amechukua hatua ya kujua hali ya afya yake ili kujikinga na magonjwa kama ya shinikizo la damu.
Aidha Sereti ameelezea kwamba akinamama wajawazito wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu kwa sababu ya mabadiliko ya hisia ya mara kwa mara huku akiichangamoto jamii ya Marsabit kuweza kuchukua tahadhari.
Mtaalam huyu wa afya ameyataja matumizi ya chumvi na mafuta ya kupikia kupindukia pamoja na kukosa kufanya mazoezi kama maswala yanayosababisha ugonjwa wa shinikizo la damu.