County Updates, Local Bulletins

ANGAZIENI PIA “BOY CHILD” -MSHAURI WA RAIS KATIKA MASUALA YA JINSIA, HARRIETTE CHIGGAI AYARAI MASHIRIKA YA KIJAMII.

JB Nateleng,

Mshauri wa Rais katika masuala ya jinsia na haki za wanawake, Harriette Chiggai amesema kuwa idadi ya wajane na akinamama wanaowalea wanao pekee yao nchini inazidi kuongozeka kutokana na jamii na mashirika ya serekali kuangazia zaidi wanawake na wasichana huku wakisahau kuhusu haki za mtoto wa kiume.

Chiggai amesema kuwa ni lazima akina wazee wachukua jukumu la kuhakikisha kwamba wamewafunza maadili mema wanao wa kiume ili kuwaepusha na matendo mabaya ambayo yanaweza dhuru maisha yao.

Chiggai ameyataja matumizi ya pombe na mihadarati na kujitosa katika sekta ya kuendesha bodaboda bila ujuzi kama chanzo cha wanaume wengi kutelekeza familia zao huku akiyachangamoto mashirika yasiyo ya kiserekali kuweza kuungana na serekali katika harakati za kuangazia masuala ya jinsia ya kiume.

Kadhalika Chiggai amewataka wanaume kuweza kuwalinda wajane na akinamama wanaowalea wanao pekee yao dhidi ya mila potovu ambayo inawakandamiza.

Aidha amesema kuwa serekali ya Kenya Kwanza inajali maslahi ya wanawake na inahakikisha kwamba kumekuwepo na usawa wakati wa ugavi wa rasilimali.

Chiggai ameelezea kwamba rais anazidi kushughulikia masuala yanayoadhiri uchumi kupitia kuboresha afya na sekta ya uekezaji.

Subscribe to eNewsletter