County Updates, Local Bulletins

AKINA MAMA WAJANE WATAKIWA KUJITOKEZA KUHESABIWA MARSABIT ILI KUHUSISHWA KWENYE MIPANGO YA SERIKALI.

Naomi Waqo – Marsabit County Women Representative

Na Samuel Kosgei

MWAKILISHI wa wanawake jimbo la Marsabit Naomi Jilo Waqo amesema kuwa kuna haja ya kujua idadi ya wanawake wajane katika jimbo la Marsabit ili kuendana na mipango ya serikali kuu na hata kuwapa usaidizi pindi panapotea misaada.

Akizungumza na meza ya Shajara, Naomi amesema kuwa akina mama wasio na mabwana ni sehemu ya jamii na hivyo kuna haja ya kuwahusisha kwenye mipango ya jimbo na hata serikali kuu.

Aidha amewataka wananchi kujitokeza kutoa maoni yao kwenye suala la kukusanya maoni leo katika harakati ya kuhalalisha hazina ya kitaifa ya maendeleo ya maeneo bunge NG-CDF na hazina ya akina mama NGAAF.

Ametetea hazina hizo akisema kuwa imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi haswa katika kuanzisha miradi ya maendeleo na kulipia watoto karo kupitia pesa za basari.

Wakati uo huo amemtaka aliyekuwa rais nne Uhuru Kenyatta kukoma na kustaafu siasa za kuwachochea vijana akisema kuwa nyingi matatizo ambayo taifa linapitia kwa sasa yamesababishwa na serikali yake alipokuwa rais. Amepuuzilia mbali miungano ya upinzani unaolenga kumwondoa rais Ruto mamlakani mwaka wa 2027.

Subscribe to eNewsletter