Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Joseph Muchai
Mwakilishi wadi wa Loiyangalani Musa Daniel Ejomo amewata wakaazi wa eneo hilo kuwa na Subira wakati huu KENHA inapojiandaa kuikarabati barabara ya Sarima Nakurol kuelekea Loiyangalani.
Akizungumza na vyombo vya habari, MCA Emojo amesema kuwa amewasiliana na mkurugenzi wa mamlaka ya barabara kuu nchini KENHA wa ukanda wa mashariki ya juu Norbat Momanyi na kukubaliana kuwa shughuli hiyo itang’oa nanga hivi karibuni.
Aidha Emojo vilevile amesema kuwa barabara hiyo imekuwa na tatizo kupitika haswa maeneo ya Nakurol kutokana na kufura kwa ziwa Turkana.
Hata hivyo amewarai waendesha magari kutafuta njia mbadala kwani kuna sehemu iliyochimbika kutokana na mafuriko hayo.