Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Ipo hoja ya kutilia maanani afya ya akili ya maafisa wetu wa usalama hapa jimboni Marsabit.
Haya yametajwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la Open Mind Focus (OMF) Bi. Mariam Abduba.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani Miriam ametoa wito kwa idara ya usalama kutumia kipindi hichi ulimwengu unapoadhimisha mwezi wa kushughulikia maswala ya afya ya akili kuangazia changamoto wanazokumbana nazo maafisa wa polisi ili kuwaepusha na hali inayowapelekea wengine wao kujitoa uhai.
Aidha Bi Mariam ametaja hoja ya hamasa kutolewa haswa kuhusiana na maswala ya afya ya akili na namna ya kupata msaada katika kaunti ya Marsabit.
Vilevile Bi. Miriam amewarai vijana kuasi utumizi wa mihadarati kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo na badala yake kufunguka na kujieleza iwapo wamekumbwa na changamoto zozozte ili wapata msaada.
Hata hivyo Bi. Mariam amepongeza hatua zilizopigwa na serekali ya kaunti katika kupambana na visa vya ugonjwa ya afya ya akili huku akiitaka serekali kuwekeza katika dawa ili kuhakikisha kwamba wanao-ugua wanapata tiba.