County Updates, Local Bulletins

WITO WA WATOLEWA KWA WAKAAZI WA MARSABIT KUJISAJILI KUPATA VITAMBULISHO; HUKU ZOEZI LA USAJILI LIKIFANYWA KIDIJITALI.

Kenyan-IDs Sample

Na JB Nateleng,

Wakazi wa Marsabit wanakila sababu ya kutabasamu baada ya mchakato wa kupata kitambulisho cha kitaifa kurahisishwa.

Kwa mujibu wa msajili mkuu katika kaunti ya Marsabit Isack Kibet ni kwamba mchakato huu umerahisishwa zaidi baada ya serekali kuu kuzindua mashine ambayo itakuwa ikikusanya maelezo ya mtu kidijitali wiki jana, hatua ambayo amesifia na kusema kuwa ni afueni kwa wakaazi ambao wamekuwa wakisubiri vitambulisho kwa muda mrefu

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Kibet ameeleza kwamba serekali inazidi kuhakikisha kwamba ifikapo mwezi wa saba mwaka huu itaboresha mchakato wa kupata kitambulisho kupitia mfumo wa kidijitali jimboni Marsabit

Kibet amewarai wakaazi wa Marsabit ambao hawajapata vitambulisho kuweza kutembelea kituo cha Huduma Center ama afisi ya kitambulisho katika maeneo walioko ili kupata huduma hii muhimu.

Wakati uo huo naibu Kamishna wa Marsabit Central David Saruni amewahakikishia wananchi kwamba mchakato wa kupata kitambulisho kwa yeyote ambaye anatafta kwa mara ya kwanza ni bure huku akiwataka wananchi kuripoti kisa chochote cha ulaghai kwa idara husika.

Kauli yake Saruni imeunngwa mkono na Adan Wako ambaye ni naibu chifu kata ndogo ya Mata Arba, kaunti ya Marsabit huku akiishukuru serekali kwa kuboresha mchakato huo kwani utasaidia pakubwa wakazi wa Marsabit kuweza kupata huduma za serekali kwa urahisi.

Subscribe to eNewsletter