County Updates, Local Bulletins

TAHADHARI YATOLEWA KWA WAKAZI WA MARSABIT BAADA YA UNGOJWA WA CHOLERA KUTIPOTIWA NAIROBI.

Picha Hisani

Na JB Nateleng,

Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa Marsabit kuhusiana na ungojwa wa Cholera ambao umeripotiwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini.

Kwa mujibu wa afisa wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Abdi Adan na ambaye ni meneja wa kituo cha kushughulikia maswala ya dharura, ni kwamba ni jukumu la wakaazi kuweza kudumisha usafi kwa kunawa mikono, kuchemsha maji na kutumia vyoo inavyofaa.

Akizungumza na idhaa hii afisini mwake, Adan amewataka wakazi kuwa makini na kuripoti kisa chochote cha ugonjwa huu kwa zahanati ama hospitali iliyo karibu nao ili hatua zinazofaa zichuliwe mapema iwezekanavyo.

Hapo jana Wizara ya Afya nchini ilithibitisha kuzuka kwa maradhi ya kipindipindu katika baadhi ya maeneo kadhaa hapa nchini.

Maeneo yaliyoathirika ni ya kaunti za Migori, Kisumu na Nairobi ambapo jumla ya visa 97 vimeripotiwa ikiwemo vifo vya watu sita.

Katika taarifa waziri wa Afya Aden Duale alitoa takwimu za kuhusiana na ugonjwa huo ambapo katika kaunti ya Migori visa 53 vya ugonjwa huo vimeripotiwa pamoja na kifo cha mtu mmoja, huku maeneo yaliyoathirika zaidi yakiwa Suna Mashariki, Suna Magharibi, Kuria Mashariki na Kuria Magharibi.

Kisumu visa vilivyogunduliwa humo ni 32, vifo vinne huku kaunti ndogo za Nyando na Muhoroni zikiripotiwa kuathirika zaidi.

Visa 12 na kifo kimoja vimeripotiwa katika kaunti ya Nairobi na maeneo ambayo yametajwa kama yaliyoathirika ni Kasarani, Kibra na Dagoretti Kusini.

Subscribe to eNewsletter