County Updates, Local Bulletins
Picha Hisani

NA JB Nateleng

Mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Marsabit na ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho ukanda wa mashariki ya juu Ali Noor ameelezea furaha yake ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo akisema kuwa ni wa manufaa kwa wakazi wa Marsabit na jamii kwa ujumla kwa sababu wataweza sasa kupata uwakilishi wa kutosha kwenye ugavi wa rasilimali wa chama hicho.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Noor amesema kuwa ni jukumu sasa la wakazi wa Marsabit kuweza kukumbatia chama hicho cha ODM kwa kujitokeza na kushiriki kikamilifu kwenye uchanguzi wa mashinani unaoendelea.

Noor ametaja upana wa eneo la Marsabit na taarifa ya kwamba chama hiki ni cha watu wa eneo Fulani pekee kuwa changamoto katika kutekeleza usajili wa wanachama jimboni Marsabit.

Hata hivyo, Noor amewahakikishia wakazi wa Marsabit kuwa chama hichoi kinajali maslahi ya wafugaji na wavuvi katika jimbo la Marsabit hivo kuwarai kujisajili kuwa wanachama ili kunufaika Zaidi.

 

Subscribe to eNewsletter