Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na JB Nateleng,
Serekali ya kaunti ya Marsabit na pamoja na serekali kuu zimetakiwa kushirikiana kuangazia masuala yanayaokumba jamii ya Loiyangalanai baada ya ziwa Turkana kufura na kuadhiri wakazi wanaoishi karibu na ziwa hilo.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, mkurugenzi wa shirika la Wong`an Women Initiative Teresalba Leparsanti amesema kuwa shule ya msingi ya El-molo Bay iliyoko eneo la El-molo eneo wadi ya Loiyangalani imeweza kuharibiwa na maji ya ziwa Turkana jambo linalotishia haki ya elimu ya watoto wa eneo hilo.
Teresalba ameelezea kuwa hali inazidi kuwa ngumu kwa wakazi wa El-molo kwani inawalazimu kuwalipia wanao nauli ya mashua ili kuweza kufika shuleni.
Teresalba ameitaka idara ya elimu katika kaunti ya Marsabit kutafuta mbinu mbadala ambazo zitahakikisha kwamba wanafunzi wa shule ya msingi ya El-molo wanasalia shuleni baada ya bweni la shule hiyo kuaharibiwa na maji.
Vilevile mtetezi huyo wa haki za binadamu ameitaka serekali ya kaunti idara ya barabara kushughulikia barabara ya kuelekea eneo la Loiyangalani ambayo pia imeharibiw ana maji ya ziwa Turkana na kutatiza shughuli za uchukuzi.
Ameyarai pia mashirika yasiyo ya kiserekali kuingilia kati na kusaidia kutatua baadhi ya maswala yanayowaadhiri wakaazi wa eneo hilo.