WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kujukumika zaidi na kuwatunza watoto wao dhidi ya maovu yanayoweza kujiri kipindi cha likizo.
Kwa mjibu ya mwenyekiti wa chama cha wazazi katika kaunti ya Marsabit, Ali Nur ambaye amezungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, amewataka wazazi kuhakikisha kwamba wanafuatilia mienendo ya wanao katika kipindi cha likizo ndefu ya mwezi Disemba.
Aidha Nur amewataka wazazi kuwahusisha watoto katika majukumu mbalimbali ya nyumbani sawa na michezo kama vile kabumbu au michezo ya kuigiza ili wasipoteze wakati wao kwa mambo yasiyofaa.
Hata hivyo Nur amewataka wazazi kufuatilia kwa ukaribu wanachofanya watoto kwa simu kwani wengine wao wanaweza kuingia katika mitandao isiyofaa au hata kujihusisha na uhalifu wa mtandao (cybercrime).